Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 09 18Article 558184

Burudani of Saturday, 18 September 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Mabasi yatakiwa kulipa Sh 50 kwa kila abiria kila wakionesha filamu za Bongo

Mabasi yatakiwa kulipa Sh 50 kwa kila abiria kila wakionesha filamu za Bongo Mabasi yatakiwa kulipa Sh 50 kwa kila abiria kila wakionesha filamu za Bongo

Dar es Salaam. Wadau  wa tasnia ya filamu Tanzania, wametaka mabasi kulipa Sh50 kwa kila abiria aliyepanda pale wanapoonyesha kazi zao katika usafiri huo.

Wametoa mapendekezo hayo leo  Ijumaa, Septemba 17, 2021 katika kikao chao na  Taasisi ya Hakimiliki (Cosota), kilichofanyika ukumbi wa Costech.

Pamoja na mambo mengine katika kikao hiko, moja ya mada iliyojadaliwa na kuwa na maoni mengi ni suala la ukusanyaji mirabaha ya kazi za famu katika mabasi ambalo linatarajiwa kuanza hivi karibuni.

Akielezea  utekelezaji wa suala hilo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Cosota, Doreen Sinare amesema kiwango kilichowekwa kwa mabasi na kukubaliana na wamiliki wake ni  Sh50,000 mabasi ambayo ni daraja la juu (luxury), daraja la kati (Semi Luxury) Sh30,000 na mabasi yanayofanya safari za ndani mikoa Sh20,000.

Kiasi hicho ambacho kitatozwa kwa mwaka, Doreen amesema wamekipitisha kama moja ya njia ya kuanzia kuwa kazi hizo zinapotumika kwenye mabasi zinapaswa kulipwa na kuongeza kuwa wataziboresha kadri watakavyopata maoni kutoka kwa wasanii wenyewe.

Wakichangia jambo hilo  kwa nyakati tofauti, wadau hao akiwemo Silvanus Mumba, amesema kiasi hicho ni kidogo ukilinganisha na gharama wanazotumia kuziandaa.

Katika mapendekezo yake Mumba ambaye pia ni Katibu wa Chama cha Waigizaji Tanzania, amesema walau kila kiti kingetozwa Sh50 na hii ni iwe wakati wote wa safari la basi usiku linapokenda naa kurudi.

Athuman Juma, ambaye ni msambazaji amesema ifike mahali wasanii wasijiweke nyuma katika kudai haki zao kwa kulipwa kidogo kwa kuwa hiyo sio hisani bali ni haki yao.

"Pia wakati tunaangalia suala hili la malipo ya mirabaha ipo haja ya kuangalia kazi hizo huko kwenye mabasi wanazipataje,maana kwa sasa ni ngumu kusimamia kwa kuwa wapo wanaozipata kwa kunyonya kwenye flash," amesema Juma.

Abdallah Shaibu, yeye alikuwa tofauti na wasanii wenzake, na kueleza kuwa ni bora waanze na kiasi hiko wakati suala hilo likiendelea kuboreshwa kuliko kuikosa kabisa, ukizingatia kuna wasanii wameshafariki na kuikosa haki hiyo na wengine hali zao ni mbaya kimaisha.

Msanii Madebe Lidali  amesema usafiri mwingine wa kuangalia ukiacha mabasi ni kwenye meli na boti kwani kote huku kazi hizo zinaonyeshwa.

Pia Madebe , amesema kuna haja ya kuliangalia suala hili la mirabaha pia upande wa Zanzibar, kwa kuwa huko wanatumia kazi zao ikiwemo kuzionyesha kwenye vituo vipya vya luninga ili kuvutia watazamaji, lakini hawajui haki zao wanazipataje.