Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 08 30Article 554299

Burudani of Monday, 30 August 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Manara atoa machozi kwa Mkapa, atambulisha mastaa Yanga

Manara atoa machozi kwa Mkapa, atambulisha mastaa Yanga Manara atoa machozi kwa Mkapa, atambulisha mastaa Yanga

MSEMAJI mpya wa Yanga, Haji Manara ametambulishwa rasmi leo kwa mashabiki wa timu hiyo na kuonekana akilia katika kilele cha Tamasha la Wiki ya Wananchi kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.

Wakati Mashabiki wa Yanga waliojaa uwanjani hapo wakisubiri kutambulishwa kwa wachezaji wao kwaajili ya msimu ujao, Haji aliingia uwanjani hapo kama ‘Sapraizi’ akizungukwa na warembo kisha kuanza kuzunguka kusalimia uwanja mzima.

Baada ya kuzunguka Uwanja Manara alienda golini na kupiga magoti akionesha kuomba kisha kuelekea kwenye jukwaa na kuonekana akitokwa na machozi.

Haji hakueleza kwanini alilia lakini moja kwa moja alishika kipaza sauti na kuanza kuwatambulisha wachezaji wa Yanga watakaotumika kwa msimu wa 2021/2022.

Katika utambulisho huo, Haji alinakshi sana majina na namna alivyowaita na kuwapokea jukwaani wachezaji wa Yanga lakini kubwa zaidi ilikua pale alipomfungia Feisal Salum kamba za viatu na kumbusu miguu.

Nyingine kali ilikua pale alipomuita beki Djuma Shaban na kusema “Aliwalaza makolo wote na viatu,” na pale alipomuita kocha mkuu wa timu hiyo Nessredine Nabi na kuongea kiarabu.

Na mwisho haji alimaliza kwa kusema “Nchi hii ina tajiri wa mpira na matajiri wa Instagram” na kuwataka mashabiki waimbe GSM.

Haji amehamia Yanga baada ya kuachana na watani zao, Simba siku chache zilizopita.