Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 08 23Article 553231

Burudani of Monday, 23 August 2021

Chanzo: eatv.tv

Mapenzi yamlevya Gigy Money, aitaka ndoa

Mapenzi yamlevya Gigy Money, aitaka ndoa Mapenzi yamlevya Gigy Money, aitaka ndoa

Ni headlines za msanii Gigy Money ambaye ameshea ujumbe wa kutamani kuingia kwenye ndoa baada ya kunogewa kwenye penzi jipya na mwanaume wake mpya.

Gigy Money ameandika ujumbe huo kupitia Instagram yake kwa kupost video clip akiwa na mwanaume wake huyo anayefahamika kwa jina la Crey.

"Mapenzi ni ujinga ndio maana sipendagi kabisa kujigusisha haya tayari nimeshapenda tena, yaani nikipenda huwa boya na mjinga kishenzi hapa najiona nina miaka miwili etiii khaaaa sitoboi"

"Tena marafiki zangu nisameheni, tulikubaliana hatumpost mpenzi 'this time but' nimeshashindwa kuficha hisia mie, si mnanijuaa napenda vibaya nisameheni tu, sema nakukubali sana mwanangu Crey"

"Tatizo sipo romantic ndio mana naibiwagwa ila kichaaa pia nimejaribu kuwa sweet uwe wa mwisho katika maisha yangu yani unioe, sio saiv miaka hata 27 huko".