Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 06 04Article 541069

xxxxxxxxxxx of Friday, 4 June 2021

Chanzo: eatv.tv

Maproducer tishio Bongo

Kama ilivyo kwa waimbaji wa muziki kila mwaka huibuliwa vipaji vipya na kupelekwa sokoni ndivyo ilivyo hata kwa watayarishaji wa muziki yaani ‘Producers’ nao huibuliwa kutokana na kazi mbalimbali za wasanii walizozifanya.

Submitted by Telesphory on Ijumaa , 4th Jun , 2021 Picha kutoka kushoto ni Producer Mocco Genius, Yogo Beats na Paul Maker

Kwa kipindi cha miaka ya hivi karibu majina makubwa ya watayarishaji wa muziki ni kama yalipotea hivi kwani kasi yao ya ufanyaji kazi ilipungua huku damu changa (vijana) zikiaminiwa na wasanii wakubwa na zikitawala soko la muziki nchini.

Baadhi ya hao ni;The Mix Killer – Alianza kusikika kwenye ku-mix kazi za wasanii mbalimbali na wengi awali wasiokuwa wakimjua vizuri walidhani ni producer Abbah, baadae kazi zake zilimtambulisha vizuri zaidi na ni mmoja wa wapishi wa album ya Darassa ‘Slave Becomes A King’.Paul Maker – Wakati watayarishaji wengine wakiwa busy na midundo ya wasanii wengi wa kuimba, yeye mikono na akili yake inawaza sana kupika hits zenye mahadhi ya Hip Hop, wasanii kama Young Lunya, Joh Makini, Salmin Swaggz na Country Boy wameishi sana kwenye ubunifu wake.Yogo Beats – Hivi sasa wengi wanamjua kama ndiye mtayarishaji rasmi wa King Kiba kwani hata kwenye safari zake za ndani na nje ya Bongo amekuwa akiongozana naye huko.

Kuwajua wengine sikiliza hapa;

Join our Newsletter