Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 09 06Article 555589

Burudani of Monday, 6 September 2021

Chanzo: eatv.tv

Marioo afunguka kuhusu kujiunga Kings na Wasafi

Marioo afunguka kuhusu kujiunga Kings na Wasafi Marioo afunguka kuhusu kujiunga Kings na Wasafi

Hit maker wa single ya Mama Amina Marioo amefunguka kwamba ofa za kujiunga na lebo ya Kings Music Records na Wasafi hazikufanikiwa kwa sababu ambazo zipo nje ya uwezo wao.

Akizungumzia taarifa hizo kupitia EATV & EA Radio Digital, Marioo amesema.

"Ukizungumzia Kings Music na Wasafi ni lebo kubwa sana East Africa na Africa kwa ujumla, lakini hizo ofa hazijawahi kutokea na hata kama zimetokea hazikufanikiwa kwa sababu ambazo zipo nje ya uwezo wetu".

Pia Marioo anasema sasa hivi hana mpango wa kusainiwa lebo yoyote hapa Africa ila anapenda jinsi Kings, Wasafi na Konde Gang wanavyofanya kazi kwa wasanii wake.