Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 09 26Article 559744

LifeStyle of Sunday, 26 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Mastaa Kenya wenye umri mkubwa tofauti na mionekano yao

Mastaa wa Kenya ambao umri wao ni mkubwa tofauti na muonekano wao Mastaa wa Kenya ambao umri wao ni mkubwa tofauti na muonekano wao

Wanawake huchukulia suala la kuzeeka kwa uzito mkubwa, na mara nyingi huficha umri wao kwa sababu za kibinafsi au za kijamii.

Lakini kuna baadhi ya Wanawake ambao umri wao husogea kila kukicha lakini bado husimama na kujiweka katika mazingira ua ujana.

wafuatao ni mastaa watano ambao wana umri wa miaka 40 na zaidi ambao ukiwaangalia wanaonekana vijana kuliko umri wao halisi. Wapo katika nyanja za siasa, burudani na tasnia ya uandishi wa Habari.

Kuwa maarufu huja na changamoto za aina mbali mbali, huku watu ikiwalazimu wengine kila wakati kuchagua kwa makini wanachovaa na jinsi watakavyoonekana.

1. Esther Musila

Esther Musila hivi karibuni alizungumziwa sana na vyombo vya habari baada ya kuibuka madai ambayo baadaye yalithibitishwa kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mwimbaji wa nyimbo za Injili Guardian Angel.

Tofauti yao katika umri iliwaacha wengi vinywa wazi juu ya lengo katika maisha yao ya kimapenzi. Walakini, ni jinsi mwili wa Musila ulivyo na mwonekano wake mzuri unaowafanya watu kuongea zaidi kuwahusu.

Ana umri wa miaka 51 lakini huonekana bado binti mchanga sana kwa umri wake. Anavaa vizuri ili kuendana na mwili wake na zaidi ya hayo, mara kwa mara amewaonyesha mashabiki wake ratiba yake ya mazoezi yanayomfanya kuendelea kuonekana kijana.

2. Akothee

Mama ya watoto watano hivi karibuni ametimiza miaka 40, na anaendelea kuhakikisha afya ya mwili wake inaimarika kila siku.

Akothee pia kupitia mitandao ya kijamii huwaonyesha mashabiki wake mazoezi mazito ambayo yeye hufanya ambayo humsaidia kuendelea kuonekana msichana licha ya umri wake.

Licha ya idadi ya watoto alionao, staa huyo anaonekana msichana sana na mwenye nguvu na ndio maisha yake.

3. Julie Gichuru

Staa huyo katika nyanja ya Uandishi wa Habari, ana watoto watano, lakini bado huonekana kama kijana.

Yeye hutumikia malengo ya mwili kwa jinsi anavyovaa, anavyoishi kwa mazoezi na kuhakikisha maisha yenye afya tele.

4. Esther Passaris

Mwakilishi wa Kike wa Kaunti ya Nairobi amekuwa gumzo siku baada ya siku kulingana na sera zake na misimamo yake juu ya masuala tofauti tofauti.

Huonekana msichana licha ya kuwa katika umri wa miaka 50. Passaris, ambaye ni mtu mashuhuri katika siasa.

5. Catherine Kasavuli

Mkongwe huyo wa Runinga bado huonekana mchanga na safi, na bado ana mashabiki licha ya kuwa kwenye Kamera za televisheni tangu miaka ya 90.

Hivi karibuni Kasavuli alirudi kwenye utangazaji baada ya kustaafu miaka saba iliyopita.

Uzuri wake na mtindo wake humfanya aonekane mwenye umri mdogo kuliko umri wake halisi.