Uko hapa: NyumbaniBurudani2022 01 12Article 585235

Burudani of Wednesday, 12 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Meena Ally Aonekana Kwenye Bango Marekani

Meena Ally Aonekana Kwenye Bango Marekani Meena Ally Aonekana Kwenye Bango Marekani

MTANGAZAJI wa Clouds FM, Meena Ally ametumia ukurasa wake wa Instagram ku-share furaha yake baada ya picha na jina lake kutokea kwenye moja kati ya mabango yaliyopo kwenye kitivo cha biashara nchini Marekani Times Square.

“Ukiangalia kwenye bango kule nyuma unaweza kuniona pale na jina langu na bendera ya Tanzania ????????! Hili bango lipo times square, a major commercial intersection in the world!

Yaani hata ningeota ndoto za aina gani nisingewahi kuota hata siku moja kwamba sura yangu itakaa hapo ???????????? ila Mungu akitaka kupa, hakika hakuandikii barua, Namshukuru sana.

Nimecheka sana nikiwaza jinsi gani times square napaonaga kwenye movies na tv ila leo na mimi niko kwenye bango hapo ???????? Hata siku moja usidhani Mungu hakuoni kwenye haya maisha ????” Ameandika meena Ally katika ukurasa wake wa Instagram.