Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 08 15Article 551644

Burudani of Sunday, 15 August 2021

Chanzo: eatv.tv

Mesen Selekta ahamia kwenye Baikoko

Mesen Selekta ahamia kwenye Baikoko Mesen Selekta ahamia kwenye Baikoko

Producer Mesen Selekta amesema ukimya wake kwenye game umesababishwa na kubuni aina mpya ya muziki ambao ni baikoko kutoka Tanga na kidumbaki kutoka Pemba, Zanzibar.

Mesen Selekta anasema muziki huo kwa pamoja utaitwa jina la kiduba na wasanii wengi watauimba kama alivyoanzisha ladha ya muziki wa singeli kwenye BongoFlava.

"Kuna project zangu nahitaji kuzileta ndio maana kuna ukimya nilikuwa nabuni aina ya muziki mwingine nataka kuuleta, ni taste ya muziki wa Tanzania kutoka makabila mawili kuna baikoko kutoka Tanga na kidumbaki kutoka Pemba Zanzibar" amesema Mesen Selekta