Uko hapa: NyumbaniBurudani2022 01 12Article 585157

Tabloid News of Wednesday, 12 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Mfungwa apeta uraiani kwa miaka 13, alipogundulika akaachiwa huru

Mfungwa apeta uraiani kwa miaka 13 Mfungwa apeta uraiani kwa miaka 13

Mfungwa mmoja huko Missouri nchini Marekani ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka 13 jela kwa kosa la wizi wa kutumia silaha mnamo mwaka 2000 , amekuja kugundulika kuwa alisahaulika kufungwa kwa kipindi chote hicho cha miaka 13 mpaka siku aliyotakiwa kuachiwa.

Hii ina maana kuwa hakuwahi hukaa gerezani hata siku moja kwa miaka yote aliyotakiwa atumikie kifungo jela.

Baadae alipokamatwa Anderson ameachiwa huru na Jaji Terry Lynn Brown wa Missouri kwa tabia njema kwa sababu kwa kipindi chote alichokaa uraiani amekuwa raia mwema, Baba , Mume bora na mlipa kodi mzuri.