Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 04 12Article 533107

Filamu of Monday, 12 April 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Miaka tisa bila Kanumba, hatua bado zile zile za kinyonga

Miaka tisa bila Kanumba, hatua bado zile zile za kinyonga Miaka tisa bila Kanumba, hatua bado zile zile za kinyonga

Kifupi ni kwamba bi mkubwa anakubalika na Wabongo asilimia 90. Hizo asilimia 10 waachie wachawi. Yes! Uchawi siyo mpaka ubebelee tunguri, hata kumchukia mtumishi wa watu bila sababu ni sehemu ya uchawi. Yaani unamchukia mtu, ukiulizwa sababu za kumchukia unaitikia “Basi tu!” huo ni uchawi pia.

Sasa watu sampuli hiyo wapo. Ndio tunawaachia zigo la misumari la kujitesa kwa ujinga wa kumchukia Bi Mkubwa. ‘Madam Prezdaa’, kakubalika Bongo, duniani mpaka mbinguni. Tangu aapishwe tu raia namba moja. Hata hali ya hewa imebadilika. Lile joto la kibwege Dar limekatika ghafla.

Hata ukienda baa siku hizi watu wanakunywa kwa ustaarabu. Bila hata kulazimishwa na kale katangazo ka ‘kunywa kistaarabu’. Hata lugha za makondakta zimebadilika. Unaweza kushindwa kutofautisha kati ya kondakta na mwinjilisti wa pale ufufuo na uzima.

Ukitaka kujua nguvu ya mama, tembelea hata mitandaoni. ‘Chatingi’ za Wabongo unaweza kudhani pengine wao ndio waandishi wa Zaburi, ufunuo wa Yohana mpaka waraka wa Mtume Paulo kwa Wakorintho. Lugha tamu, nzuri, sahihi na yenye staha. Hiyo ndio zama ya mama kama mama. Ogopa sana mwanangu mwenyewe. Wacha tudeke huku tukipiga mzigo.

Ukiona kiongozi kawabadilisha watu kifikra bila kutumia nguvu wala msukumo wowote. Yaani basi tu watu kwa wingi wao wamebadili fikra na wanaishi kiungwana. Ujue huyo kiongozi aliletwa duniani na Mungu ili awaongoze. Amefanya mpaka wadangaji wajitundike ushungi kwenye michongo yao. Uliza!!!

Ni swaga hivi sasa. Mama anaenda sawa na lugha za mtaa, lugha za Bakita, lugha za kwenye nyumba za ibada mpaka ung’eng’e wa Kitrump Trump. Mama la mama siyo mtu poa, ohoo!!! Ukizingua mtazinguana. Hili taifa lilihitaji tiba na faraja zaidi kuliko utajiri wa mtu mmoja mmoja.

Ukipita Kariakoo kila mtu anatabasamu. Ukiwa mgeni unaweza kuuliza hili ni soko au ukumbi wa harusi? Watu wana amani na furaha kama vile wameahidiwa kupelekwa peponi kesho asubuhi. Amazing sana. Mama akaletwa na Mungu.

Kama ulikuwa unakatika stimu sana na mizinguo ya neno kwio hiyo kwio? Basi usikonde limeisha hilo! Halizimii kinomanoma na alishawachana wanaolitumia. Kwamba neno kwio kitambo hicho wao walijua ni kuku. Tofauti na matumizi yake ya sasa. Lakini si unajua mama la mama kwake zege halilali? Ole wenu muendelee kuzingua na kwio hiyo kwio.

Pia ‘Madam Prezdaa’ aliwaonya waandaaji wa ‘muvi’ na vichekesho. Kuwataka watumie maneno ‘propa’. Kwamba michongo yao ndio inaongoza kwa husambaza fasta misemo ya kindezi. Kifupi ni kwamba kuna lugha mtaa na za kibwege hataki kabisa kuzisikia.

Kumbuka wakati anaonya hapo alikuwa msaidizi tu, na Hayati JPM ‘Chuma’ akiwa ndio steringi. Leo hii yeye ndio mshika mpini mwenyewe. Sijui kama umeelewa? Utamwambia nini? Zingua akuzingue. Twende tumsaidie bi mkubwa kujenga nchi na utaifa. ‘Ishu’ zingine zitaenda sawa tu msikonde.

Ukitaka kujua balaa la mama. Hata msela kutoka kipande cha Uchingani Chingani huko, Harmonize a.k.a Konde Boy, na pisi yake yenye asili ya Kanda ya Ziwa Kajala binti Masanja. Spidi ya ‘Madam Prezdaa’, imewatoa kwenye ramani ya ‘kutrendi’ kindezi. Na sasa wanahaha ile mbaya kurudisha mizuka yao. Dizaini wamefubaa sana na kiki zao hazitembei kama mwanzo.

‘Trendi’ ya ‘Prezdaa’ Samia, imekuwa ‘hevi weiti’ kinyama. Kiasi cha kuzima kiki zote kitaa kuanzia Bongo Movie na Bongofleva, wote wameamua kunyuti kama makinda ya ndege kupisha upepo upite. Lakini Konde Boy na Kajala wanataka kupimana na ‘pawa’ ya bi mkubwa sijui. Wapendwa hawa ambao wameamua kujenga penzi kwa nguvu ya ‘shoo offu’ mitandaoni. Hapo kati wamezuga kumwagana, lakini kiki ikabuma. Wakasambaza stori kuwa Konde Boy kamtokea mtoto Paula kwa ‘esemesi’ na bi mkubwa akainasa, waapi mchongo ukabuma. Kajala na Paula siku hizi ‘wanajishuti deile’ wakicheza au kusikiliza pini za Wasafi, lakini waapi ‘trendingi’ yao mitandaoni ni ‘ziro pointi ziro ziro iziko tu ziro’.

Wameshindwa kusoma ramani. Kwamba bi mkubwa ni noma kinoma, na asilimia 90 ya Wabongo wanamzimia kinyama. Wananchi wanataka kusikiliza stori na hotuba zake tu. Kaenda wapi na nani anamzingua ili wazinguane naye.

Timu ya Simba pamoja na mafanikio yao lakini bado ‘trendi’ ya bi mkubwa wameshindwa kuifunika kabisa. Mama anakimbiza kinoma, na ole wao afanye mkutano sehemu. Hakuna mtu wa kusombwa hata na kirikuu, tutajaa na utajua hujui.

‘Ene wei’ ngoja tuachane na ishu za bi mkubwa kidogo. Ujue wiki hii Machi 7 ilikuwa siku ya mapumziko yaani Karume Day. Kumbukizi ya kifo cha mwamba wa Mapinduzi matukufu ya Zanzibar, Abeid Aman Karume. Lakini pia ndiyo siku ambayo miaka tisa iliyopita tulimpoteza msela wetu Steven Kanumba. Yes!

Jamaa alikuwa anajua kufanya kazi yake. Na ‘of coz’ alikuwa staa kwa maana ya ustaa. Katika wakati wake bora kabisa, akiwa juu ya kilele haswa. Alifanya hata wabunge na mawaziri watamani kuwa yeye. Angekuwa hai mpaka leo, naamini wasanii wengi wangejiingiza Bongo Movie badala ya kwenye singeli. Kumbuka hata baadhi ya wale waigizaji wenzake walitamani kuwa yeye.

Jamaa aliacha alama kubwa sana kwenye sanaa ya filamu. Alifanya vitu vya mbele kuliko wakati wao. Yaani alikuwa hatua nyingi mbele kuliko tasnia ya filamu Kibongo Bongo. Wakati hivi sasa waigizaji wanalia ukosefu wa soko la kazi zao. Kanumba angekuwa anawaza jinsi ya kuwatonya washikaji zake wa Gabon, Mali sijui Nigeria na kwingineko juu ya ujio wa filamu yake mpya.

Jamaa alisafiri Mashariki, Kaskazini, Magharibi na Kusini kutangaza kazi zake. Leo hii tungewaona kina Aunty Ezekiel wapya wa kutosha. Alimuingiza Wema, Lisa Jensen, Jokate, Uwoya, Kajala na wengineo kibao kwenye filamu. Achana na wale watoto kina Jennifer na filamu ile ya ‘Uncle JJ’. Kila kijana alitamani kuigiza kama Kanumba. Hakuna aliyetamani soka wala muziki.

Hata heshima wanayopata wasanii wa sasa kwa viongozi wa kiserikali ni kutokana na uzito wa mazishi ya Kanumba na wenzake. Umati wa mazishi yao uliwaamsha viongozi na kuwajulisha kwamba wasichukulie poa. Maisha bana. Leo hii kila kijana anataka kuwa Nandy au Rayvanny. Hata waigizaji wanataka kuwa Konde Boy.

Join our Newsletter