Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 11 23Article 573643

Burudani of Tuesday, 23 November 2021

Chanzo: millardayo.com

Mkali wa Amapiano kutoka SA ameachia EP yake, mtanzania apata shavu

Mkali wa Amapiano kutoka SA ameachia EP yake, mtanzania apata shavu Mkali wa Amapiano kutoka SA ameachia EP yake, mtanzania apata shavu

Ikiwa bado Afrika Kusini wanaendelea kuchukua vichwa vya habari hususani kupitia muziki wao unaopeta kwasasa kwenye chart mbalimbali.

Sasa Good news nyingine ninayotaka kukupatia ni kwamba mkali Musa Keys ambae ni mtayarishaji & DJ ameachia Ep mpya iitwayo TAYO.

Kwenye EP hiyo mpya iliyobeba ngoma zisizopungua tano amesikika pia msanii kutokea Bongo Flevani, Loui.

Loui ni msanii mpya kutokea kwenye kiwanda cha Bongo Flevani ambae mpaka sasa ameshafikisha miezi sita tangu atambulishwe rasmi kusimamiwa kazi zake chini ya lebo  Legancy Record.

Kupitia collabo hii aliyofanya na Musa Keys huenda ikamuongezea wasikilizaji wapya hususani wale wapenzi wa muziki wa Amapiano.

Unaweza ukabonyeza play kusikiliza kile alichokiimba Loui pia usisahau kuandika neno lolote ili mkali huyo akipita asome mlichomuandikia.