Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 05 10Article 537055

xxxxxxxxxxx of Monday, 10 May 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Mke wa Profesa Jay aingiza miguu ndani ya filamu

Grace Mgonjo ambaye ni mke wa msanii Profesa Jay, ameingiza miguu kwenye filamu, ambapo sasa ataonekana katika tamthilia ya ‘We Men’. Hayo yamebainika jana Jumapili Mei 9,2021 katika uzinduzi wa tamthilia hiyo, itakayokuwa ikionyeshwa kwenye kisimbuzi cha StarTimes. Akizungumza na Mwanaspoti, Grace ambaye pia ni mshehereshaji,  amesema alikuwa na ndoto ya kuigiza siku nyingi, lakini alikuwa hajapata filamu ambaye ameona inamfaa.

“Kiukweli ndoto za kuigiza nilikuwa nazo siku nyingi, sema tub ado nilikuwa naangalia filamu gani naweza kuigiza na We Men nimeona ni saizi yangu ndio maana nikakubali kushiriki,” amesema Grace. Kwa upande wake Profesa Jay ambaye alikuwa ameambatana na mke wake huyo mwanzo mwisho, amesema tangu mwaka 2009 anajua kiu ya mke wake huyo kwenye filamu na asingeweza kumkataza kwa kuwa Sanaa ina faida yake na ndio imemvusha sehemu nyingine hadi kuwahi kuwa Mbunge. “Kwangu sanaa naiheshimu, na ninaheshimu kipaji cha mtu, hivyo kwa mke wangu kuingia huko kwenye filamu sioni tabu, kwani zote ni Sanaa. Ni kutokana na hilo, amesema hata yeye anatarajia kuingia huko, ambapo mipango ni kutengenezea filamu baadhi ya nyimbo zake zilizofanya vizuri huko nyuma ikiwemo zali la mentali na nyinginezo. Katika filamu hiyo, mbali na Grace, yupo Wema Sepetu, Shilole, Max Rioba na Hemed Suleiman.

Join our Newsletter