Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 06 18Article 543352

Burudani of Friday, 18 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Msanii Bahati ajibu mapigo 'Pete Yangu' kuhusishwa na wizi

Msanii Bahati ajibu mapigo 'Pete Yangu' kuhusishwa na wizi Msanii Bahati ajibu mapigo 'Pete Yangu' kuhusishwa na wizi

Msanii Kelvin Bahati wa nchini Kenya amejibu shutuma dhidi yake zikimhusisha na wizi wa wimbo wa mwimbaji kutoka Rwanda, Butera Knowless.

Madai hayo yanaeleza kuwa wazo la wimbo mpya wa Bahati unaotambulika kwa jina ‘Pete Yangu’, aliomshirikisha msanii Nadia Mukami, limetokana na wimbo ‘Peke Yangu’’ wa Msanii Butera Knowless, aliouachia miaka mitano iliyopita.

Akijibu tuhuma hizo, Bahati amenukuliwa akisema: ‘’ukiwa namba moja, wa mwishoni watakuonea wivu na kukuchukia kwa sababu hawaelewi kwanini Mungu amekuchagua wewe na sio wao’’.

Mjadala huo unaozungumzia utata juu ya wimbo huo umeenda mbali zaidi kwenye kulinganisha midundo ya wimbo huo na ule wa Knowless huku ikidaiwa kuwa kuna ulinganifu sambamba na mtiririko wa mashairi.

Hivi sasa, kibao hicho ‘Pete Yangu’ kinavuma katika mtandao wa YouTube kwani tayari watazamaji 908,476 wameshautazama wimbo huo ikiwa ni siku tatu tu zimepita tangu upakiwe kwenye mtanadao huo.