Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 06 03Article 540736

LifeStyle of Thursday, 3 June 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Mtoto wa Komba Ashushiwa Kipigo na Polisi, Chanzo Mkewe

Mtoto wa Komba Ashushiwa Kipigo na Polisi, Chanzo Mkewe play videoMtoto wa Komba Ashushiwa Kipigo na Polisi, Chanzo Mkewe

Mtoto wa Komba Ashushiwa Kipigo na Polisi, Chanzo Mkewe – Video June 3, 2021 by Global PublishersMTOTO wa aliyekuwa mbunge wa Mbinga Magharibi (CCM) na mwimbaji maaarufu wa nyimbo za siasa nchini Tanzania, hayati Kapteni John Komba, Michael Komba amedai kupewa kichapo cha mbwa koko na baadhi ya polisi wa Kituo cha Magomeni kwa tuhuma za kufanya fujo kituoni hapo.

Akizungumza na GLOBAL TV mwishoni mwa wiki jijini Dar, Michael alisema tukio aliloita ni la kikatili alitendewa na askari hao kisha kuwekwa mahabusu kwa siku moja.

Akisimulia mkasa huo, alidai kuwa licha ya kwamba kitaaluma ni mwanasheria, pia anamiliki saccos ambayo hukopesha watu mbalimbali kuanzia Sh 100,000 hadi Sh milioni 20.

Alisema siku ya tukio alikwenda kuchukua fedha za mkopo ambazo alimkopesha mmoja wa askari katika kituo hicho ambapo askari huyo alichukua fedha na kuweka bondi gari yake aina ya IST.

Join our Newsletter