Uko hapa: NyumbaniBurudani2022 01 14Article 585886

Burudani of Friday, 14 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Mwijaku Adai Harmonize Ndio Icon ya Muziki wa Bongo Flava Tanzania

Mwijaku na Harmonize Mwijaku na Harmonize

Kutoka kwa mtangazaji na mwanamitandao maarufu Instagram kama DC wa insta @mwijaku_01 ameshare andiko ambalo limemtaja mwanamuziki @harmonize_tz kama icon /alama/ nembo ya muziki wa Bongofleva.

Mwijaku ametumia ukurasa wake wa Instagram kuandika andiko hilo refu katika maadhimisho ya miaka 58 ya mapinduzi ya zanzibar ,huku akimwagia sifa msanii huyo ambae ndie mmiliki wa record label ya KondeGang na kuelezea kuwa anastahili kupewa sifa akiwa hai.

mwijaku_01 #2022-Rajab Abdul Kahali , Uncle "KondeBoy" Life begins at forty .Mfalme Solomoni alipata kusema,"Marafiki wengi waweza kumuangusha mtu lakini wapo marafiki waaminifu kuliko ndugu. @harmonize_tz

Katika siku ya kumbukizi ya mapinduzi ya zanzibar, najivunia kuwa na rafiki anayeniambia ukweli machoni kwangu na kunisifia kwa watu bila mimi kuwepo.

Busara zako,hekima na moyo wako wa unyenyekevu wako wa kujifanya dhaifu wakati ni shujaa,ni haiba bora kwako na pambo maridhawa linaloitimisha utu wako katika maisha yako,na mafanikio yako.

Mwenyezi Mungu,akubariki uwe na akili ya uchumi kama Joseph wa Yakobo na mwenye imani thabiti kama Ibrahim.

Ewe ICON wa mziki wa BongoFleva, uzima na afya yako katika kumbukizi ya siku ya mapinduzi ya zanzibar leo ni ishara kwamba Mungu bado ana kusudi nawe kukufundisha jambo na kupanda mbegu kwenye nafsi za watu.

Unastahili kupewa sifa ukiwa ungali hai,kwa kuweka utu wako kwa jamii, lipe hadhi jina lako kwani litakubakia, litadumu kuliko hazina elfu moja za dhahabu za maharamia na vibaraka wao.

Wakati wa furaha ni wa muda tu ,lakini jina zuri hudumu milele. You are my right hand ,live life to the fullest. Black excellence... All the best Angel Investor..Rajabu Abdul kondeee JESHI

#AskMwijaku #HappyMapinduziDay