Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 09 20Article 558613

Televisheni of Monday, 20 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Mwonekano wa nywele za Patrick Kanumba washtua

Patrick Kanumba Patrick Kanumba

MWIGIZAJI maarufu Bongo Movies, Patrick Kanumba ameshtua wengi baada ya kuonesha mwonekano wake mpya wa nywele kama mwanamke.

Patrick Kanumba ameshea picha zake akiwa saluni na mchekeshaji Dulivan (Da Zuu) ambaye anatuhumiwa kumharibu kwa sababu wamekuwa wakifuatana sehemu mbalimbali.

Maoni ya wengi ni kwamba hajapendeza kwani mwonekano huo unamuondolea mwonekano wa kiume kwa kumfanya kuonekana kama mdada kutokana na kuweka dawa kwenye nyweli na kusuka kama wanawake.

Baada ya maoni kuwa mengi, Patrick Kanumba akaposti picha na video za mkali Ronaldo na Diamond Platnumz wakiwa na nywele kama yeye.

Patrick Kanumba alipata umaarufu akiwa mdogo alipokuwa akiigiza na aliyekuwa kinara wa Bongo Movies, Kanumba aliyetangulia mbele ya haki.