Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 08 17Article 551932

Burudani of Tuesday, 17 August 2021

Chanzo: eatv.tv

Mzee Yussuf achaguliwa kuwa Makamu wa Rais

Mwimbaji Taarab, Mzee Yusuff Mwimbaji Taarab, Mzee Yusuff

Mkali wa taarab wa muziki Bongo Mzee Yussuf amepata uongozi wa kuwa Makamu wa rais wa shirikisho la muziki Tanzania.

Mzee Yussuf amesema amegombania na amefanikiwa kupata uongozi huo ambao unalengo la kutoa fursa, sapoti na bima kama msanii akiuumwa na kusaidiwa.

"Mimi ndiyo makamu wao wa rais wa shirikisho la muziki wote, vyama vya BongoFlava, taarab na kwaya ndiyo unatengeneza muziki wote, nimegombania nimepata" amesema Mzee Yussuf

Aidha ameongeza kusema watanzania wapunguze choyo na ubinafsi kwenye kusapotiana kwenye masuala ya kazi kwani yanarudisha nyuma maendeleo ya kufika mbali.