Uko hapa: NyumbaniBurudani2022 01 07Article 583975

Burudani of Friday, 7 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Nadia Ajibu Kuhusu Ujauzito

Nadia Ajibu Kuhusu Ujauzito Nadia Ajibu Kuhusu Ujauzito

Mwanamuziki kutoka nchini Kenya Nadia Mukami ameelezea kusikitishwa kwake na maneno aliyoyatoa mtangazaji maarufu wa redio nchini humo Jalango.

Akiyazungumzia mahusiano ya kimapenzi ya msanii huyo hadi kujikuta akitoa siri za ndani, kinyume na matakwa ya Nadia, wakati wa kipindi chake cha asubuhi ambapo alidai kuwa msanii huyo alikuwa akificha ujauzito wake na mwanamuziki Arrow boy.

Baada ya kusambaa kwa kasi kwa taarifa hizo, Nadia aliutumia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram kuchapisha video akisimulia alivyoumizwa na kitendo cha Jalango kuvujisha taarifa zake zisizopaswa kuwekwa hadharani.

Akimzungumzia Jalango, Nadia alisema kuwa alichokifanya mtangazaji huyo ni kitendo cha ajabu.

"Ulichofanya ni makosa kabisa, kusema ukweli. Nisingejali, hata kama wewe ni mtu wa blogu, mtangazaji au shabiki. Lakini ulitualika nyumbani kwako, ili ufungue mdomo wako na kinachofuata ni kuhalalisha makosa uliyoyafanya na kusema haujutii,” alisema Nadia.

Nadia Mukami aliendelea kweka wazi kwamba yeye na Arrow Bwoy wamepitia mambo mengi katika maisha yao ambapo wameamua kuweka mambo yao binafsi kuwa siri hivyo kitendo cha Jalango kuvujisha taarifa za ujauzito wa Nadia na Arrow boy kumetafsiriwa kama kuwakosea heshima kwa kujivika mamlaka ya kuwa msemaji wa familia yao.