Uko hapa: NyumbaniBurudani2022 01 14Article 585802

LifeStyle of Friday, 14 January 2022

Chanzo: dar24.com

Nandy aukana ujauzito

Nandy na Bill Nas Nandy na Bill Nas

Mwanamuziki mahiri wa muziki wa Bongo fleva, Faustina Charles Mfinanga, maarufu Nandy amekanusha madai ya kwamba ana ujauzito wa mpenzi wake msanii Billnass, licha ya kuenea kwa kasi juu ya taarifa za mwanamuilziki huyo kuwa na ujauzito.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukabidhiwa ubalozi wa moja ya makampuni nchini, mwimbaji huyo aliweka wazi kuwa hatarajii, na kuongeza kuwa atakapopata ujauzito habari hizo hazitafichwa kwa mashabiki wake.

“Kwa sasa hamna ujauzito, na mimi kama unafuatilia swala la uja uzito, huu ni mwaka wa pili sasa ninazungumziwa.

Nakumbuka wakati nikifanya nyimbo za Giza Kinene, nimeshiba zangu watu wakasema nina ujauzito. Sasa Uja uzito gani huo ambao haukui, wala sizai ?

Watu waache kupredict vitu, na nikiwa na ujauzito hakuna kitu cha kuficha⁣.” Alisema Nandy.

Nandy amekua kenye uhusiano na Mwanamuziki mwenzake Billnass kwa takriban miaka 2 sasa.