Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 09 19Article 558325

Burudani of Sunday, 19 September 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Nandy kwake hela kwanza, sura sio ishu

Nandy kwake hela kwanza, sura sio ishu Nandy kwake hela kwanza, sura sio ishu

Ule usemi wanaoujiliwaza nao waja wanapoelezwa kuwa na sura mbaya kwa kusema kama ni sura, hata mbuzi anayo, sasa umetua kwa msanii wa Bongofleva Nandy.

Hii ni baada ya jana Septemba 17, 2021 , mkali huyo wa kibao cha ‘Nimekuzoea’ kupitia InstaStory yake kuandika ujumbe kuwa bora awe mbaya ila awe na hela.

Nandy ambaye jina lake halisi ni Faustina Charles, katika ujumbe wake huo aliweka picha ikimuonyesha amesuka rasta ndefu na kuzibana katikati. Usoni mwake hakuwa amepaka make up yoyote  kama alivyozoeleka.

Kisha akaandika ”Nimepost picha makusudi tu uone wanawake walivyo wachawi, utasikia kumbe ndio ulivyo hivyo kama hawakujui vile au ndio picha ya kwanza wameiona.

“Tafuteni hela unatakuiwa useme kumbe ndio hela  ulizonazo hizo,unahukukumu sura, upuuzi mtupu. Mimi ni bora niwe mbaya ila niwe na hela, chaaaa,"