Uko hapa: NyumbaniBurudani2022 01 14Article 585787

Burudani of Friday, 14 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Nay Mitego: Nimechoka Kuulizwa Kuhusu Diamond

Nay Mitego: Nimechoka Kuulizwa Kuhusu Diamond Nay Mitego: Nimechoka Kuulizwa Kuhusu Diamond

Ushkaji wa Diamond na Nay wa Mitego mara nyingi umekuwa ukisemekana kuingia dosari na hii inatokana na wawili hao kutoonekana pamoja kwa muda mrefu wala hakuna hata mmoja kati yao anaye support harakati za mwenzie.

Hawa ni washkaji ambao walikuwa wameiva sana na kufikia hatua ya kuachia kolabo mbili ambazo zilifanya poa sana way back ambazo ni Muziki gani na Mapenzi Pesa.

Ghafla ushkaji ukapungua na hadi leo haijulikani nani alimpunguza mwenzie, na Hakuna hata mmoja kati yao aliyewahi kukiri kuwa na ugomvi na mwenzake.

Hasa kupitia EFM Kwenye pindi la Empire hii jana Jan 13, Nay amedai katika maswali ambayo hapendi na amechoka kuyaongelea ni kuulizwa kama bado anaongea na Diamond,alicho kiongea ni kuwa ibaki tu kuwa kikubwa kila mmoja ana mishe zake na zinasonga.

Nay Amefunguka haya baada ya mtangazaji Jonijoo kutaka kujua kama bado wana ukaribu na Diamond kama ilivyokuwa zamani.