Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 08 18Article 552163

Burudani of Wednesday, 18 August 2021

Chanzo: eatv.tv

"Niliigiza huku nanyonyesha" - Monalisa

Muigizaji Monalisa Muigizaji Monalisa

Happy Birthday to Yvonne Cherrie Monalisa ambaye anatimiza miaka 40, na ameshea story kwamba wakati anaigiza kwa mara ya kwanza huku anamnyonyesha mwanae Sonia akiwa mtoto mchanga kabisa.

Monalisa ameshea story yake hiyo kwenye kumbukumbu ya kuzaliwa kwake kupitia page yake ya Instagram ambapo ameandika kuwa

"Nilianza kujulikana na Watanzania miaka 21 iliyopita kama Muigizaji nikiwa na umri wa miaka 19 kama umri huu alionao sasa binti yangu Sonia Monalisa"

"Filamu yangu ya kwanza girlfriend niliigiza huku nikiwa namnyonyesha binti huyu akiwa mchanga kabisa, Look at us now twinning hakika siku hazigandi"

Aidha Monalisa ameongeza kuwa "Kesho ndugu zangu rasmi naingia floor ya 4, huwezi amini, tofauti na wanawake wengi ambao wanaogopa ukubwa"