Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 07 05Article 545464

Burudani of Monday, 5 July 2021

Chanzo: eatv.tv

"Nimekuja DSM na ndege sio gari" - Barakah

"Nimekuja DSM na ndege sio gari" - Barakah

Ni mbwembwe za msanii Barakah The Prince ambaye ametusanua kwamba wakati anaingia jijini Dar es Salaam kwa mara ya kwanza kutokea Mwanza alitumia usafiri wa ndege na sio gari kama walivyofanya wasanii wengi kutoka mikoani.

Submitted by Shaluwa Anta on Jumatatu , 5th Jul , 2021 Msanii Barakah The Prince

Barakah The Prince amesema hilo kupitia EATV & EA Radio Digital, baada ya Tundaman kumwambia alimsaidia nauli ya kuja Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya ishu za kimuziki.

"Mimi sikuja Dar kwa bus nimekuja na ndege mtafute mama Bob Junior ndiye alikuja kunipokea Airport na gari lake, ila Tundaman alinisaidia kunipa Tour yake wakati anafanya show Mwanza, kipindi hicho ana wimbo wake na Spark na hakuna aliyekuwa hatamani kukutana naye" amesema Barakah The Prince

Mengine zaidi aliyoyazungumza Barakah The  Prince kuhusu safari yake ya kufika Dar mtazame hapo chini kwenye video akieleza zaidi.