Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 11 21Article 573193

Burudani of Sunday, 21 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Offset Amkaribisha Kaka Yake Baada Ya Miaka 15 Gerezani

Offset na kaka yake Offset na kaka yake

Rapa kutoka kundi la Migos, Offset amemkaribisha nyumbani kwa furaha kaka yake ambaye alifungwa gerezani tangu mwaka 2006.

Kitu cha kwanza ambacho Offset alimfanyia kaka yake ni kumpeleka saluni kwa ajili ya kunyoa nywele zake, huku akimpeleka hadi nyumbani kwake ambapo alimtambulisha kwa watoto wake na mke wake Cardi B huku wakifurahi na marafiki.

Haijafahamika ni kwanini kaka huyo wa Offset alifungwa gerezani, lakini tangu mwaka 2006 alipokamatwa na kufungwa gerezani Offset alikuwa bado na umri mdogo!