Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 09 09Article 556279

Burudani of Thursday, 9 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

PICHA 4:Uzinduzi BSS msimu wa 12, Salama Jabir ndani

Tukio la uzinduzi wa BSS Msimu wa 12 Tukio la uzinduzi wa BSS Msimu wa 12

Lile Shindano maarufu na linalosifika kwa kuibua vipaji nchini Bongo Star Search maarufu kama BSS limerudi tena kwa mwaka 2021.

Usiku wa Septemba 8, 2021 umefanyika uzinduzi wake kwa msimu wa 12 ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo ambaye alipata nafasi ya kufungua zawadi ambayo ilikuwa suprise katika hafla hiyo.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na wadau mbali mbali wa masuala ya sanaa na muziki wakimwemo watangazaji na watayarishaji wa muziki.

Lakini katika tukio ambalo limewashangaza wengi ni baada ya kumuona mwanadada mtata Salama Jabir akirudi tena kama Jaji katika mashindano hayo baada ya kutoonekana kwa misimu miwili.