Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 09 07Article 555931

Burudani of Tuesday, 7 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

PICHA 4: Vanessa Mdee na Rotimi wanatarajia mtoto pamoja

PICHA 4: Vanessa Mdee na Rotimi wanatarajia mtoto pamoja PICHA 4: Vanessa Mdee na Rotimi wanatarajia mtoto pamoja

Star wa muziki aliyetangaza kuachana na muziki baada ya kudai kuwa kuna mambo mengi ya kuumiza ndani ya kiwanda cha muziki nchini Tanzania, Vanessa "Vee Money" Mdee, ametusuprise na picha zake akionesha ujauzito wake na mpenzi wake star wa filamu na muziki Rotimi.

Kupitia Instagram, Vanessa Mdee ameshare picha zake kuonesha hatua nyingine kubwa katika maisha yake. Ikumbukwe kuwa Vanessa na Rotimi wamekua kwenye mahusiano ya wazi kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.

Hivi karibuni kulizuka taarifa kuwa Vanessa ni mjamzito lakini yeye mwenyewe alikuja kuzikanusha hizo taarifa na kudai kwamba zinampa presha mama yake mzazi.

Rotimi ni mwimbaji na muigizaji mwenye asili ya Nigeria lakini anaishi na kufanya kazi zake nchini Marekani ambako anaishi pamoja na Vanessa.