Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 09 21Article 558760

Tabloid News of Tuesday, 21 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Paula, Fahyma Vita Imeanza

Fahvanny, Rayvanny na Paula. Fahvanny, Rayvanny na Paula.

MWANZONI zilikuwa ni hisia tu kwamba, huwenda aliyekuwa baby mama wa staa wa Bongo Fleva, Rayvanny ambaye amezaa naye mtoto mmoja, Fahyma ana bifu zito na mpenzi mpya wa jamaa huyo, Paula Kajala, lakini sasa ni rasmi kuna vita nzito.

Tangu Paula amekuwa mpenzi wa Rayvanny yapata miezi kadhaa sasa, hajawahi kujihusisha na mtoto wa wawili hao aitwaye Jaydan, lakini sasa amefanya hivo na kukutana na balaa la aina yake akidaiwa kumchokonoa Fahyma.

Wengi walishatabiri kwamba, endapo Paula atajihusisha na mtoto huyo kwa madai kwamba ni mama wa kambo, basi ajiandaye na mziki mzito kutoka kwa Fahyma na hicho ndicho kilichojiri.

Kitendo cha Paula kumposti mtoto huyo kwenye Insta Story yake na kuweka makopakopa, kimeelezwa kwamba kuna kitu anamtafuta Fahyma kwa sababu hapendi kabisa ajihusishe na mwanawe.

Watu wa karibu wanasema Fahyma hapendi kujibizana na Paula, lakini safari hii hawezi kuvumilia kwani huko ni kumtafuta uchokozi.

Uchunguzi umebaini kwamba, wanawake walio wengi hawapendi watoto wao kuhusishwa na wapenzi wapya wa wanaume waliozaa na kutengana nao.