Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 11 18Article 572512

Burudani of Thursday, 18 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Prof. Jay: Wasanii Hawajishughulishi

Prof. Jay Prof. Jay

Msanii guli wa Bongo Fleva, Joseph Haule maarufu Profesa jay amefunguka mtazamo wake juu ya mwenendo mzima wa tasnia ya muziki huo kwasasa, Ukilinganisha na namna ambavyo wasanii wa zamani walivyokuwa wakifanya.

Profesa amesema anachokiona kwa wasanii wengi wa sasa ni uvivu katika kufikiria na kuzalisha aina ya maudhui yenye tija kwa hadhira, jambo linalosababisha wengi wao kuishia kutengeneza nyimbo zilizo chini ya ubora na viwango na kuishi kwa muda mfupi tofauti na walivyokuwa wakifanya wasanii wa zamani ambao mpaka sasa nyimbo zao zinaishi.

''watu wanataka wepesi tu, dunia imekuwa kama kijiji, kiswahili kinapasua anga lakini pia muziki wetu kwa kiasi chake tumeanza kupasua kwenda mataifa mengine, laikini badala ya watu kufanya kitu kilichokuwa sahihi sasa hivi, watu wanataka wepesi, hawataki kuhangaika kuhusu kuandika mashahiri na kuweka ubunifu kwenye kazi zao'', amesema Profesa Jay.