Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 06 12Article 542407

Burudani of Saturday, 12 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Professa Jay awaonya wanaoimba matusi

Professa Jay awaonya wanaoimba matusi Professa Jay awaonya wanaoimba matusi

NYOTA wa muziki wa kizazi kipya Joseph Haule ‘Profesa Jay’ amewaonya wasanii wanaoimba matusi kubadilika na kuwahimiza kuzingatia maadili.

Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam juzi Profesa Jay alisema vijana wengi wanaochipukia wanaimba muziki ambao mtu akikaa na familia kuangalia ni aibu tupu.

“Hawa watoto wanaochipukia wamebadilisha muziki, wengi wanaimba matusi na mara nyingi nimekuwa nikikemea kwa sababu kuna vitu vingine ni aibu huwezi kuangalia na familia,” alisema.

Alisema sababu ya kukemea mara kwa mara wanaoimba matusi ni kujaribu kuwakumbusha kuzingatia maadili.

Katika hatua nyingine, msanii huyo alisema wiki ijayo anatarajia kuachia kibao kipya kuonesha mashabiki kuwa bado yupo.

Alisema ataendelea kutoa wimbo mmoja kila baada ya muda ili ifikapo mwishoni mwa mwaka huu awe na hazina kubwa ya nyimbo kwa ajili ya albam.

Professa Jay alisema albamu hiyo itakuwa na nyimbo atakazoshirikiana na wasanii kadhaa wa nyumbani na wengine wa nje ya nchi na hivi karibuni ataanza safari za kimataifa.