Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 11 23Article 573691

Burudani of Tuesday, 23 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Rais Samia: Konde Boy Kweli ni Tembo

Rais Samia na Harmonize Rais Samia na Harmonize

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan amesmifia staa wa muziki wa Bongo Fleva, Harmonize kutokana na performance ambaye ameifanya leo jijini Arusha.

Mhe. Samia amesema hayo wakati akihutubia mara baada ya kushuhudia shoo kali ya Harmonize na H-Baba kwenye hafla ya Wiki ya Nenda kwa Usalama ambayo Rais Samia alikuwa mgeni rasmi.

"Nimemuona pia Konde Boy Tembo hapa (kwenye orodha ya wasanii waliotoa burudani) na kwa kifua kile kweli yeye ni Tembo, kwa vikundi vyote vingine vilivyopanda hapa jukwaani kwa burudani tunawashukuru kwa ujumbe kuhusu upunguzaji wa ajali,"- Rais Samia leo, Arusha.