Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 11 23Article 573697

Burudani of Tuesday, 23 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Rais Samia: Muulizeni Marioo 'Kwa Nini Hanywi Bia'

Rais Samia na Marioo Rais Samia na Marioo

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan amesmifia staa wa muziki wa Bongo Fleva, Marioo kutokana na performance ambaye ameifanya leo Novemba 23, 2021 jijini Arusha.

Mhe. Samia amesema hayo wakati akihutubia mara baada ya kushuhudia shoo kali ya Marioo na kundi lake kwenye hafla ya Wiki ya Nenda kwa Usalama ambayo Rais Samia alikuwa mgeni rasmi.

"Tumemsikia Marioo hapa ingawa Marioo anawaambia wenzie ule unywaji ni mtamu (Bia Tamu) lakini yeye hanywi, kwahiyo muangalie vizuri hapa anayekupa meseji akakisifia kitu na yeye afanye kama yeye hafanyi muulizeni kwanza kwanini?" - Rais Samia, leo Arusha.