Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 10 10Article 562444

Burudani of Sunday, 10 October 2021

Chanzo: eatv.tv

Rais Samia kayasema haya kuhusu Diamond, Alikiba na Nandy

Rais Samia kayasema haya kuhusu Diamond, Alikiba na Nandy Rais Samia kayasema haya kuhusu Diamond, Alikiba na Nandy

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za kuwapongeza wasanii wa BongoFlava Diamond Platnumz, Alikiba, Nandy, Rosa Ree, Marioo na Zuchu kwa kuchaguliwa kuwania tuzo za AFRIMMA 2021.

Rais Samia amewapongeza wasanii hao 6 katika Uzinduzi wa Kampeni ya Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa kupambana na Uviko19 kwa kusema tuwape moyo, tuwaunge mkono na tuwapigie kura kwa wingi ili kuweza kushinda tuzo hizo.

Pia amempongeza bondia Hassan Mwakinyo na timu ya wanawake Twiga Stars kwa kuchukua ubingwa wa COSAFA siku ya jana.