Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 09 10Article 556711

Burudani of Friday, 10 September 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Rapcha aachia albam ‘Wanangu 99’ kupitia Boomplay

Rapcha aachia albam ‘Wanangu 99’ kupitia Boomplay Rapcha aachia albam ‘Wanangu 99’ kupitia Boomplay

MSANII wa Hiphop nchini Tanzania, Cosmas Paul Mfoy almaarufu ‘Rapcha’ ameachia album yake ya kwanza iliyopewa jina la ‘Wanangu 99’ kupitia streaming platform namba moja ya muziki barani Afrika, Boomplay.

Rapcha anaachia albam hiyo ndani ya kipindi cha miezi mitatu tu baada ya kuachia ngoma yake ya ‘Lissa’ ambayo inaendelea kufanya vizuri na kushika chati za juu za muziki wa Bongo fleva.

Wimbo huo una zaidi ya watazamaji milioni 1.5 kwenye mtandao wa YouTube.

‘Wanangu 99’ ni album ya kwanza ya msanii Rapcha yenye jumla ya nyimbo 10 ambazo ni Majani, Go Rapcha, Unaua vibe remix, Nitakucheki, Kama unae, Tunajimwaga, Wanangu, Mungu na masela, Lissa I na Lissa II.

Katika albam hiyo, Rapcha amewashirikisha wasanii wanne ambao ni Femi One, King Kaka, Mapanch BMB na Kid GoldenAlbam.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa albam hiyo, Rapcha ambaye kwa sasa yupo chini ya usimamizi wa ‘Bongo Records’ alisema “Nyimbo zote zilizomo kwenye albamu yangu zinazungumzia baadhi ya vitu ambavyo mimi binafsi nimevipitia katika maisha yangu halisi.

“Kupitia albam hii, nataka mashabiki wangu wamuelewe Rapcha ni nani, kitu ambacho kimenisukuma kutengeneza albam ambayo nina uhakika wa asilimia 100 mashabiki zangu wataipenda”.” alisema

Kwa upande wa Muanzilishi na Mkurugenzi wa Lebo ya ‘Bongo Records’, Paul Matthysse al-maarufu P-funk ambaye pia ni Meneja wa msanii huyuo alisema “Katika kipindi kifupi, Rapcha ameweza kuwa moja ya wasanii wakubwa wa Hiphop nchini Tanzania, ameachia ngoma kali ambazo zimevunja rekodi ya chati mbalimbali za muziki wa Bongo.” alisema

Alisema ana uhakika kupitia albam hiyo Rapcha anaenda kuwa msanii namba moja wa Hiphop nchini Tanzania.