Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 10 11Article 562600

LifeStyle of Monday, 11 October 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Rasmi WhatsApp ya kiswahili yaanza kutumika

Rasmi WhatsApp ya kiswahili yaanza kutumika Rasmi WhatsApp ya kiswahili yaanza kutumika

Mtandao wa kijamii wa WhatsApp umeanza rasmi kutumia lugha ya Kiswahili ili kuwasaidia watumiaji wa lugha hii kuweza kutumia vizuri mtandao huo.

Hii inatajwa kama hatua nyingine muhimu katika kukuza lugha ya kiswahili ambayo hadi sasa ina zaidi ya watumiaji milioi 200 wengi wakiwa katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Huduma inapatikana katika nchi zote ambazo zinatumia lugha hii kama vile Tanzania, Kenya, Uganda , Rwanda na DRC.

Mtandao huu sio wa kwanza kutumia lugha hii, mitandao kama Facebook, Twitter na Google inatumia kiswahili kwa muda mrefu sasa.

Facebook ilianza kutumia kiswahili mwaka 2005 na Twitter mwaka 2016.Matumizi ya kiswahili yalianza mara baada ya watumiaji wa mitandao hii kutoka nchini Kenya kujaza maombi maaluum ya mtandaoni kama sehemu ya kushinikiza matumizi ya lugha ya kiswahili.

Mtandao wa Google wenyewe ulienda mbele zaidi, kwa kuweka vipengele vya lugha za asili kama kichaga, kisukuma, kihehe, kizaramo ili kuwarahisishia watu wote nafasi ya kupata taarifa na kujua yanayoendelea duniani.