Uko hapa: NyumbaniBurudani2022 01 13Article 585376

Burudani of Thursday, 13 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Rayvanny Ampigia Chapuo Tulia Uspika wa Bunge

Rayvanny Ampigia Chapuo Tulia Uspika wa Bunge Rayvanny Ampigia Chapuo Tulia Uspika wa Bunge

Mwanamuziki na mmiliki wa record label ya Next Level Music ‘NLM’ Raymond Mwakyusa 'Rayvanny', ameonekana kumuunga mkono Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Tulia Ackson' kwenye mbio za kuwania nafasi ya kitu cha spika wa Bunge la Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania.

Kupitia insta story ake VannyBoy ameshare picha ya mbunge huyo wa Mbeya Mjini na kuandika; “WHY NOT” akimaanisha kwanini isiwezekane kwa mgombea huyo wa kiti cha uspika wa bunge kushinda katika kinyang'anyiro hicho.

Mpaka sasa watu zaidi ya 30 wameshachukua fomu kwa ajili ya kuchuana katika kinyang'anyiro hicho ili kumpata mrithi wa aliyekuwa Spika wa Bunge, Job Yustino Ndugai ambaye alijiuzulu wiki iliyopita.