Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 09 03Article 555211

Burudani of Friday, 3 September 2021

Chanzo: eatv.tv

Recho kazungumza kuhusu wanaosema Shilole apunguze mwili

Recho aibuka na mwili wa Shilole Recho aibuka na mwili wa Shilole

Msanii Recho Kizunguzungu ametoa comment yake kuhusu mwili wa Shilole ambao umekuwa gumzo mitandaoni kwa kusema kunenepa au kupungua ni jinsi mtu mwenyewe anavyotaka.

Akizungumzia hilo kupitia show ya DADAZ ya East Africa TV Recho anasema 

"Kwenye suala la unene, kunenepa au kupungua ni mtu mwenyewe anavyotaka, Shilole anaishi na mume wake na mumewe ameridhika mbona hajamwambia aende gym au aende China akajipunguze, ameridhika na mwanamke wake" 

Recho Kizunguzungu ameongeza kusema kwamba hawezi kuishi maisha ambayo anapangiwa na watu bali anaishi anavyotaka yeye.