Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 11 24Article 573904

Burudani of Wednesday, 24 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Rekodi nyingine ya JAY Z kwenye tuzo za GRAMMY

Jay Z Jay Z

Rapa Jay Z kwa amefanikiwa kuweka rekodi mpya kwenye tuzo za Grammy baada ya kufikisha idadi ya kutajwa mara 83 kwenye vipengere mbalimbali vya tuzo hizo.

Hii ni kufuatia Jay Z kutajwa tena kwenye vipengele vitatu kwenye tuzo za Grammy mwaka 2022, akiingia kupitia kolabo ya ngoma iitwayo 'Bath Salts' aliyofanya na marehemu DMX pamoja na Jail aliyoshirikiana na Kanye West.

Kipengele kingine kinaihusu album ya Kanye West Donda ambayo Jay Z ameshiriki pia. Jay Z sasa amemzidi mtayarishaji wa muziki mkongwe mwenye umri wa miaka 80 Quincy Jones.