Uko hapa: NyumbaniBurudani2022 01 11Article 585010

Burudani of Tuesday, 11 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Rick Ross ATena kwa mobetto

Rick Ross ATena kwa mobetto Rick Ross ATena kwa mobetto

BAADA ya kumchunia na kusababisha mwanamama Hamisa Mobeto kusemwa kuwa ametoswa na rapa wa Marekani, Rick Ross, hatimaye jamaa huyo ameanza tena kujikomba kwa mwanamitindo huyo.

Tangu mwishoni mwa mwaka jana na mwanzoni mwa mwaka huu, Rick Ross ambaye baadhi ya Wabongo wanamuita Mpoki alikuwa kimya, lakini wikiendi iliyopita amerejea na kuanza kumsifia upya Hamisa baada ya kuona video yake inayomuonesha akinyonga mauno kiufundi.

Baada ya Hamisa kuposti video hiyo ndipo Rick Rossakaibuka na kuweka emoji za motomoto kama zote, jambo linalotafsiriwa kwamba jamaa amerejesha majeshi.

Mwaka jana, Hamisa na Rick Ross walikutana Dubai na kula bata kama lote ambapo baadhi ya mashabiki wamwanamitindo huyo wa kimataifa za Tanzania waliamini wangeenda mbali zaidi na kuwa mke na mume.