Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 06 14Article 542656

Burudani of Monday, 14 June 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Rick Ross, Hamisa kwenye anga nyingine

Rick Ross, Hamisa kwenye anga nyingine Rick Ross, Hamisa kwenye anga nyingine

NI wiki ya pili sasa kumekuwepo na kufuatiliwa kwa ‘post’ za mwanamitindo, Hamisa Mobetto na comment anazozitoa rapa wa Marekani, Rick Ross.

Rapa huyo ambaye jina lake halisi ni William Leonard Roberts II, alijizolea umaarufu kupitia vibao mbalimbali ikiwemo Sorry, Money Dance, The Devil is a Lie na ule wa Onyinye alioshirikishwa na kundi la P-Square.

Hivi karibuni alijikuta midomoni mwa wabongo baada ya kuonekana akiwa anatoa maoni kwenye post mbalimbali katika ukurasa wa Hamisa huku baadhi wakisema kuwa tayari wawili hao wapo kwenye mahusiano ya kimapenzi.

Wakati watu wakidhania hivyo, chanzo cha karibu na familia ya Mobetto kinaanika yote yanayoendelea kati ya wawili hao huku kikiomba kisitajwe jina lake.

Iko hivi. Rick Rose na Mobetto kwa mara ya kwanza walifahamiana baada ya kupata dili la kutangaza kinywaji cha Belaire.

Unaambiwa baada ya Rick ambaye kwenye Instagram anatumia jina la Richforever, kumwona mrembo huyo akavutiwa naye na kumwendea DM.

Katika maswali ya hapa na pale si akataka kumjua kiundani yeye ni nani, anafanya nini na Hamisa naye bila kuremba akafunguka yote.

“Yaani Rick alipojua Hamisa ni msanii anayeimba na kuigiza akazidi kudata na kumtaka amrushie baadhi ya nyimbo alizowahi kuimba.

“Haukupita muda jamaa akamwelewa na ndio hapo akamwomba afanye naye kolabo, yaani jamani kuna watu wana bahati zao, msanii kama yule mkubwa yeye ndiye atake kufanya kolabo, mwenzetu mbona ndio katoboa hivyo,” kilisema chanzo hiko.

MENEJA WAKE AFUNGUKA

Mwanaspoti ilimtafuta Meneja wake, Dk Ulimwengu, kumuuliza kuhusu jambo hilo kama lina ukweli.

Majibu yake ilikuwa ni tusubiri hapo baadaye kuona kinachoendelea kwani sasa hivi ni mapema sana kulizungumzia suala hilo.

Alipoulizwa kama ana mahusiano naye, alisema hawezi kuzungumzia jambo hilo kwa kuwa huwa hausiki na mahusiano ya mrembo huyo na hayo ni maisha yake binafsi yeye anachodili naye ni ishu za kazi tu.