Uko hapa: NyumbaniBurudani2020 10 04Article 511201

Burudani of Sunday, 4 October 2020

Chanzo: HabariLeo

Rosaree atamani kuolewa

Rosaree atamani kuolewa

MWIMBAJI wa hip hop, Rosaree Robert amesema moja ya vitu anavyotamani katika maisha yake ni kuolewa na kuwa na familia.

Msanii huyo alibainisha hayo jana Dar es Salaam katika mahojiano yake na Clouds Media akijibu maswali mbalimbali ya mashabiki wake.

“Moja ya ndoto zangu kubwa ni kuja kuwa mama wa watoto wa kike na kiume,” alisema msanii huyo ambaye leo anatarajia kukiwasha Element katika tamasha la muziki la kimataifa.

Rosaree anatarajiwa kupanda jukwaa moja na msanii wa kimataifa wa Nigeria, Divine Ikubor ‘Rema’.

Mbali na ndoto hiyo, kingine anachokiwaza alisema huenda huko baadaye akawashika wasanii chipukizi mkono lakini kabla hajakimbilia huko, lazima apate elimu ya kutosha ili ajue cha kufanya asije kuwapoteza.

“Nimewahi kuwaza namna ya kuwashika mkono chipukizi, kila kitu kinahitaji mpangilio na kila kitu kina muda wake, lazima nipate elimu ya kutosha ili nikimshika mtu mkono nijue kitu cha kufanya, wapo wengi wakali na kuna wengine nimewahi kufanya nao kazi,”alisema.

Join our Newsletter