Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 10 10Article 562363

Burudani of Sunday, 10 October 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Rubani: Wema Yupo Moyoni Mwangu

Wema na Rubani Dunkan Wema na Rubani Dunkan

RUBANI wa ndege kubwa wa Kitanzania ambaye pia ni msanii wa Bongo Fleva, Danzak ameweka wazi kwa mara nyingine baada ya ukimya wa muda mrefu kwamba, staa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu bado yuko moyoni mwake na anampenda mno.

Danzak anasema kuwa, kwa sasa yupo kimya, lakini siyo kwamba amemsahau Wema.

Anasema kuwa, Wema ni mwanamke ambaye yupo moyoni mwake siku zote na anamuombea heri, azidi kufanikiwa kwa lolote analoomba kwa Mola wake.

“Sijamsahahu, bado yupo kwenye moyo wangu, nampenda sana na ninamuombea kwa Mungu amfanikishie katika kila jambo ambalo analifanya kwenye maisha yake.

“Najua Wema anajua ni jinsi gani ninampenda na hilo ndilo muhimu sana kwake kulikumbuka,” anasema Danzak ambaye aliwahi kutajwa kutaka kumchumbia Wema, lakini mambo hayakwenda sawa.