Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 09 04Article 555337

Burudani of Saturday, 4 September 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Salama Jabir Aacha Kazi EATV, Simba Yatajwa

Salama Jabir Aacha Kazi EATV, Simba Yatajwa Salama Jabir Aacha Kazi EATV, Simba Yatajwa

Mtangazaji nguli nchini na kipenzi cha wengi, Salama Jabir jana alitangaza kuachana na kituo cha EATV ambacho amefanya kazi hapo kwa muda wa takribani miaka 19 huku sababu kuu ikiwa ni kwenda nje ya media hiyo kuona pia hali ikoje.

Salama amekuwa EATV kwa muda mrefu akijizolea umaarufu zaidi na vipindi kama Mkasi ✂, Shabiki On Saturday (SOS) pamoja na kipindi cha SALAMA NA..

Lakini tetesi zimekuwa nyingi mitandaoni kuwa uwenda akawa msemaji wa klabu ya Simba SC japo mwenyewe amekataa kuwa si kweli na yeye anaziona habari hizi kwenye mitandao ya kijamii kama tunavyoona sisi.

Lakini tayari imeshaelezwa kuwa Salama kwa sasa anafanya kazi kwenye Kampuni MultiChoice kupitia king’amuzi chao cha DStv.