Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 08 16Article 551755

Burudani of Monday, 16 August 2021

Chanzo: eatv.tv

Serikali kurudisha Tuzo kwa wasanii

Waziri wa habari na utamaduni,sanaa na michezo Mhe. Innocent Bashungwa Waziri wa habari na utamaduni,sanaa na michezo Mhe. Innocent Bashungwa

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Innocent Bashungwa amesema Wizara yake imerudisha tuzo za muziki na sanaa mbalimbali ambazo zitafanyika mwishoni mwa mwaka huu 2021.

Waziri Bashungwa amezungumza hilo kupitia show ya DADAZ ya East Africa TV ambapo amesema "Tumerudisha tuzo za kila mwaka na mwaka huu mwishoni tutakuwa na tuzo na mambo mengi yaliyokuwa na faida huko nyuma chini ya uongozi wa Rais Samia tunayarudisha, tuzo za muziki na sanaa mbalimbali vyote vinarudi".