Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 11 20Article 573046

Burudani of Saturday, 20 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Shilole Ajirudi Kwa Kiba

Shilole na Kiba Shilole na Kiba

Wiki kadhaa zilizopita, mwanamama Shilole alikinukisha mno kupitia Wasafi, akimpaka msanii King Kiba baada ya kusema kuwa hakumualika kwenye pati yake ya usikilizaji wa albam yake mpya ya Only One King.

Lakini usiku wa kuamkia Jumamosi, Shilole huyohuyo ametumia jukwaa la Clouds kujirudi kwa Kiba akiomba watu wapigiwe ngoma ya jamaa huyo inayokwenda kwa jina la Jelous.

Ishu hiyo imeibua mjadala kwa watu walioamini kwamba Shilole hawezi kusogelea au kujihusisha na muziki wa jamaa huyo.

Wengine wanasema ukiona ndugu wanagombana, chukua jembe ukalime, wakipatana nenda ukavune.