Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 09 20Article 558523

Burudani of Monday, 20 September 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Sholo Mwamba aipongeza serikali tamasha la Tanzanite

Sholo Mwamba aipongeza serikali tamasha la Tanzanite Sholo Mwamba aipongeza serikali tamasha la Tanzanite

MSANII wa muziki wa singeli, Sholo Mwamba ameipongeza serikali kwa wazo la kuandaa tamasha la michezo kwa wanawake kitaifa.

Tamasha hilo la Tanzanite, lilianza Alhamisi iliyopita na kumalizika juzi kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika.

Akizungumza na gazeti hili baada ya kutumbuiza kwenye tamasha hilo juzi, Sholo alisema ni kubwa na lenye faida kwani linawakutanisha wanawake kutoka maeneo mbalimbali ili kujumuika pamoja na kufurahi.

Alisema anaamini muendelezo wa sherehe hizo kwa miaka ijayo utakua mzuri zaidi kwani pamoja na kwamba limefanyika kwa mara ya kwanza, lakini lilikuwa na mvuto wa hali ya juu.

“Naamini huu ni mwanzo, mwendelezo wake utakua mkubwa zaidi kwani kama mwanzo wake tu watu wameupokea vizuri na watu wamefanikiwa kufanya biashara nyingi kupitia tamasha hili hivyo kesho na kesho kutwa litakua kubwa zaidi ya hili,” alisema Sholo.

Mbali na Sholo, wasanii wengine waliotumbuiza kwenye tamasha hilo ni Frida Amani, Khadija Kopa, Lwiza Mbutu kutoka bendi ya muziki wa dansi ya Twanga Pepeta.

Wengine ni Hellen George ‘Ruby’, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’, Rosa Ree na Faustina Charles ‘Nandy’