Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 08 08Article 550174

Filamu of Sunday, 8 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Siku 90 baada ya kuondolewa, Slay yarudi Netflix

Mwigizaji Mtanzania, Idris Sultan Mwigizaji Mtanzania, Idris Sultan

Hatimaye filamu ya ‘Slay’ aliyocheza Mtanzania, Idris Sultan na wenzake kutoka nchi mbalimbali Afrika imeweza kurejea kwenye mtandao wa Netflix tangu iondolewe Mei 2, 2021.

Filamu hiyo iliwekwa Netflix Machi 26 mwaka huu, huku Idris akiweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza nchini kuingiza filamu kwenye mtandao huo mkubwa duniani kwa mauzo ya filamu.

Sababu ya kutolewa ni kutokana na kukiuka taratibu za hakimiliki ambapo filamu hiyo imetumia wimbo uitwao ‘All For You’ wa msanii, Wendy Shay kutoka Ghana bila makubaliano yoyote na mmiliki wa nyimbo hiyo.

Baada ya suala hilo kumalizika ndani ya miezi, Netflix wameirejesha filamu hiyo kwenye jukwaa lake.

Ukiachana na Idris, filamu hiyo ina wakali kama Tumi Morike, Ramsey Nouah, Fabian Adeoye Lojede, Enhle Mbali, Amanda Du-Pont, Lillian Dube na wengineo wengi.