Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 09 18Article 558196

Tabloid News of Saturday, 18 September 2021

Chanzo: Habarileo

Sina mahusiano Botion - Amber Lulu

Msanii wa BongoFleva 	Amber Lulu Msanii wa BongoFleva Amber Lulu

Baada ya kusambaza video na picha akiwa ameumia usoni kwa madai ya kupigwa na mzazi mwenzake mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya, Lulu Euggen Amber Lulu amesema kwa sasa hayupo tena kwenye mahusiano na mwanaume huyo.

Amber Lulu ambaye anatamba na wimbo wa Nipost, amesema hawezi kumkataza mzazi mwenzake kuja kumuangalia mtoto, hivyo anapokuja hapo ni kwaajili ya kumuangalia mtoto wao Arianna.

Amesema lakini kuhusu mahusino hana mtu, hivyo watu wasimuulize maswali yoyote yupo na nani au kuhusiana na mzazi mwenzake kwakuwa tayari ameshatangaza hadi kwenye mitandao ya kijamii kwamba hayupo kwenye mahusiano.

“Stakiiii jamani sijarudiana na mtu na haitokuja kutokea ishapita huko kabisa najutaa,” amesema.