Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 08 26Article 553945

Burudani of Thursday, 26 August 2021

Chanzo: eatv.tv

'Sisi ni maarufu OG sio wa IG" - Ferooz

'Sisi ni maarufu OG sio wa IG 'Sisi ni maarufu OG sio wa IG" - Ferooz

Hitmaker wa ngoma ya starehe Ferooz amewachana wasanii wa sasa wasiosapoti kazi za wakongwe kwa kusema wao ndio wana umaarufu wa ukweli kuliko wasanii ambao wanaupata Instagram.

Ferooz amefunguka kusema kibongobongo tayari ameshamaliza na hata umaarufu wao ni Original 'Og' na sio umaarufu wa Instagram 'IG' na followers wa wasanii wa sasa ambao Insta ikifa nao wanakufa.

Ferooz anasema wasanii wa sasa wanavimba kusapoti kazi za baadhi ya wasanii wa zamani kwa sababu ya kibiashara na wanawahofia wakiwapa sapoti watakuwa wanawapa nafasi.