Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 09 19Article 558295

Burudani of Sunday, 19 September 2021

Chanzo: millardayo.com

Str8uplive imerudi kivingine, kuinogesha Dar es Salaam

Str8uplive imerudi kivingine, kuinogesha Dar es Salaam Str8uplive imerudi kivingine, kuinogesha Dar es Salaam

Najua Nina watu wangu wanaopenda burudani hususani kupitia muziki wa live sasa nina habari njema ninayotaka kukujuza ni kwamba kuna vijana zaidi ya saba wenye utashi mkubwa ambapo wameungana kwa pamoja ili kuhakikisha Muziki wa bendi ufike mbali kimataifa

Kundi hilo liitwalo  Str8uplive linaundwa na wakali watano akiwemo Zungu The Drummer, DJ Skadi,  na wengineo.

Miongoni mwa vitu wanavyofanya wakiwa jukwaani wakali hao kutumia vyombo vya muziki na kuubadilisha wimbo wa msanii kuwa wa tofauti kwa kutumia vyombo hivyo hivyo vya muziki.

Akizungumza na Millardayo.com & Ayo TV mmiliki wa bendi hiyo alisema ‘Kundi hili lina miezi kadhaa tangu limeanzishwa na mpaka sasa tumeshafika Mwanza, Arusha pia hapa Dar es Salaam tuliweza kuonesha uwezo wetu na utofauti wetu na bendi zingine ni kwamba muziki unaopigwa wowote na vijana hawa wanatumia Ala za Muziki kuonesha uwezo walionao’– Sniper Mantana

‘Lengo letu ni kutaka nchi yetu inapata heshima kupitia muziki wa bendi naamini kuna siku watu wataamini ninachosema haijawahi kutokea hiki kinachofanywa na hao vijana ambao kila mmoja ana uwezo wake wa kitofauti’- Sniper Mantana

‘Mpaka sasa tumeshafanya shows Mikoa ikiwemo Arusha, Mwanza, Dar es Salaam na mapokezi si ya kitoto na vile tulivyotarajia kiukweli tunawashukuru mikoa hiyo tuliyopita na kuhusu mikoa  mingine wakae karibu na mitandao yetu ya kijamii  Str8uplive ambapo tutakuwa tukiwapa habari mbalimbali’- Sniper Mantana

Kundi hilo usiku wa leo Septemba 18, 2021  litawaburudisha watanzania pale Elements Masaki Dar es Salaam.