Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 06 09Article 541705

Burudani ya

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Sukari ya Zuchu yawapagawisha wanawake Dodoma

Sukari ya Zuchu yawapagawisha wanawake Dodoma Sukari ya Zuchu yawapagawisha wanawake Dodoma

Dodoma. Msanii wa Bongofleva, Zuchu amewapagiasha wanawake katika mkutano wa wanawake wa Mkoa wa Dodoma na Rais Samia Suluhu Hassan na wimbo wake wa Sukari.

Mkutano huo unaofanyika Leo Jumanne Juni 8 2021, ambapo Rais Samia anazungumza na wanawake nchini kupitia wanawake wa mkoa wa Dodoma.

Zuchu alipanda stejini akiwa na wachezaji wake kadhaa alionyesha kulitawala jukwaa kwa yeye kucheza kwa zaidi ya dakika 20.

Hata baada ya kumaliza kuimba wimbo huo wanawake walisikika wakitaka aendelee kutumbuiza hadhara hiyo kwa nyimbo nyingine.

Pia Zuchu ameongoza wanawake wa mkoa wa Dodoma kuimba wimbo maarufu wa Super women.

Hatua ambayo ilimfanya kuendelea kuimba nyimbo nyingine huku baadhi yawatu wakimfuatisha kuimba na kucheza.

Join our Newsletter